Jamii kujitawala, kujiwezesha na kujiendeleza
Maneno muhimu
U
DeutschEnglish version of this documentLa versión española de este documento.La version française de ce document.KiswahiliRussian VersionRussian Version
HindiHindi
..
Ugomvi wa kitabaka:
...
Hii ni dhana iliyotumiwa na Karl Marx, katika jamii za kiviwanda, na ugomvi kati ya wenye navyo na wasio navyo (wanaouza nguvu zao kwa wenye navyo ili waweze kuishi). ........ Katika jamii yako kama mwezeshaji katika jamii wa wakulima, utawaona wenye navyo katika uzalishaji kama wamiliki ardhi (kama ilivyo kabla ya viwanda) na wakulima, vibarua au manamba.
.
Katika jiji kama mwezeshaji hutaona mwenye nacho yoyote anayemiliki viwanda au mali, ila utaona wafanyakazi na wapangaji katika makazi ya hali ya kipato cha chini.
.
(Deutsch: klassenkampf, English: class conflict, Español: lucha de clases. Français: conflit de classe, Português: conflito de classe, Pyccкий: Классовое Противоречие).
Uhodari:
...
Uhodari ina maana ya ushujaa, Na niushujaa si kwa kufanya jambo gumu bali kwa kulifanya kiusahihi, kama vile kuwa mwaminifu na muwazi katika pesa za kikundi au jamii. . Pia ni chanzo cha neno "tia moyo", kituambacho wewe kama mwezeshaji utakuwa unajaribu kukifanya, kuwasisimua ili waache uchoyo na ubinafsi na wajiingize zaidi katika kazi za kuisaidia jamii na jinsi kiongozi mzuri anavyotakiwa kuwa.
.
(Deutsch: mut, English: courage, Español: ánimo, Français: courage, Português: coragem).
..
Ujinsia:
.
Neno"ujinsia" linatumika katika kutofautisha aina mbili za maneno "kiume" na "kike."
.
usichanganye na neno "jinsia"ambalo linatumika katika kutofautisha "mwanaume" and "mwanamke."
....
Ujinsia na namna ya kutafsiri nini maana ya kiume na kike inatofautiana kati ya tamaduni na tamaduni, na kati ya jamii na jamii.
.
Nia yetu kuhusu ujinsia ni kuona jinsi gani inaweza kuathiri mgawanyo wa madaraka, uhusiano kiuchumi, na tofauti za kijamii.
....
Hii ni mojawapo ya jambo muhimu linaloathiri jamii na pia linaathiri kazi ya mwezeshaji.  . Mwezeshaji lazima (pia ni moja ya hitaji la kusoma kuhusu jamii) kuelewa thamani, muelekea na maadili yanayoizunguka jamii husika. 
...
Mwezeshaji pia anafanya kazi katika kupunguza tofauti iliyopo kisiasa na kiuchumi kati ya jinsia, kama kiungo muhimu katika uwezeshaji. Angalia moduli ya ufundishaji Ujinsia.  Ujinsia Umri, Rangi, na Jinsia.
.
(Deutsch: gender, English: gender, Español: género, Filipino/Tagalog: pangkasarian o kasarian, Français: genre, Kiswahili: ujinsia, Português: género, Romãnã: gen, Somali: Jandar)
Ukarabati wa kijamii:
...
Ukrabati hapa unamaanisha mazingira (kibaiolojia), hisia au kiakili (au urudishaji) wa watu ambao wameathirika kiuwezo kimwili, kimawazo au kiakili. . pale ambapo ukarabati ni wa kijamii basi maamuzi yote na majukumu ya wakuwasaidia wote walioathirika ni ya jami na hayaanzii nje ya jamii.
,
Angalia ufupisho, CBR.
.
 (Deutsch: gemeindenahe Rehabilitation, English: community based rehabilitation, Español: rehabilitación basada en la comunidad, Français: Réhabilitation communautaire, réadaptation a basé dans la communauté, Português: reabilitação baseado na comunidade).
..
Uongozi:
...
Neno Neno ni neno pana zaidi ya neno serikali.
.
Si rasmi na inahusisha zaidi sheria katika maana yake.
....
Inamaanisha namna nzima ya kufanya maamuzi, menejimenti ongozi, uratibu na nguvu ya uongozi katika muundo wowote kama jamii. ... Uongozi bora ni uaminifu ushirikishaji,uwajibikaji, uwazi, uendelevu, usawa, demokrasia, kuheshimu watu wote na kuwatumikia.
.
(Deutsch: Regierungsführung, English: governance, Español: administración, Français: gouvernance, Português: governação, Somali: hogaanka).
Ushiriki wa jamii:
..
Ushiriki wa jamii ni ziadi ya kuchangia pesa, au nguvu ya kazi, au vifaa, ni kushiriki katika kufanya maamuzi kuchagua mradi wa jamii, kupanga, kutekeleza, kutawala, kudhibiti, na kuongoza. inatofautiana na mchango wa jamii. . Ramsa ya kijamii inaendeleza shughuli za jamii huku ikiwa katika nafsi ya jamii kuchukua majukumu zaidi kwa maendeleo yake, kuanzia maamuzi ya mradi upi wauchukue na kuangalia namna ya kukusanya mali ghafi kwa ajili ya mradi husika.
.
ushirikishwaji wa jamii unahakikisha kuwa maamuzi yanayo husu mradi yanafanywa na wanajamii wote. (sio wachache) au watu toka nje.
.
Katika njia hii, mchango wa jamii unasaidia watu kujisitoa kwa hali na mali katika mradi sababu wanaushirika nao. PIa tunazishauri serikali na wafadhili wake kuzihusisha jamii husika katika kupanga miradi yao. . Ushirikishwaji wa jamii hapa usichukuliwe kama mbadala wa michango ya jamii. (kama inavyofanywa na watu wengi kimakosa); Ushiriki hapa una maanisha kushiriki katika kufanya maamuzi, kuongoza na kuchunga.
.
(Deutsch: gemeindepartizipation, English: community participation, Español: participación comunitaria, Français: participation de la communauté, Português: participação da comunidade, Somali: Ka Geyb Galka Bushada).
...
Ushupavu:
...
Ushupavu ni moja ya elementi kumi na sita za nguvu, uwezo, au nia ya jamii au ushirika.  Angalia: ELementi za nguvu ya jamii.  ikiwa inasilishwa kibinafsi ni kiasi gani watu wanashiriki katika ushupavu kama jamii.  mfano katika kuamini kuwa jamii inaweza kupata/kufanya jambo fulani. . mitizamo chanya, nia, ushawishi binafsi, mshawasha, maono, kujitegemea na si utegemezi, nia ya kupigania haki, kutokuwa wabinafsi na wachoyo, na maono ya nini kinawezekana. Kuongezeka nguvu inamaana ya kuongezeka ushupavu.  Unapokuwa unaihamasisha jamii kufanya jambo fulani, mwezeshaji unatakiwa kufahamu kazi ya ushupavu katika kuiwezesha jamii au ushirika.
...
(Deustch: zuversicht, English: confidence, Español: confianza, Français: confiance, Português: confiança).
..
Usugu:
..
Usugu ni moja ya aina tano za umasikini na utegemezi
..
Wakati mwingine huhusihwa na filosofia ya kifo Muombe Mungu lakini pia jisaidie" kwa kirusi msemo, unasema kuwa tuko kwenye mikono ya Mungu, lakini pia tuna majukumu yetu binafsi. .. Tumeumbwa na uwezo mwingi: kuchagua, kushirikiana, kupanga, na kuinua viwango vya maisha yetu; tusimtumie Mungu kama njia ya kukwepa kufanya kazi.
.
(Deutsch: Apathie, English: apathy, Español: apatía, Filipino/Tagalog: pagsasawalang bahala, Français: apathie, Kiswahili: usugu, Português: apatia, , Romãnã: apatie, Somali: naceyb)
.
Utamadunisho:
..
Neno "utamadunisho" ni jinsi au namna ya kujifunza utamaduni mpya, tofauti na enculturation.
.
mara nyingi humaanisha kwenda kwenye jamii mpya ambapo tamaduni ni tofauti, lakini pia ni sehemu ya mazoea ambayo tunayahitaji kwa ajili ya kuzoea mabadiliko katika jamii zetu (nina maana ni endelevu) zinazotuzunguka. . Kazi yako kama mwezeshaji itatoa matokeo ya mabadiliko ya jamii (maendeleo)katika jamii. wanachama kwenye hiyo jamii ni lazima"wajitamadunishe" (wajizoeshe) kwenye jamii mpya.
.
Angalia majadiliano ya wanafunzi katika maingiliano[socialization).
.
(Deutsch: akkulturation, English: acculturation, Español: aculturación, Français: acculturation, Italiano: , Português: aculturação).
..
Utawala binafsi:
..
"Utawala binafsi"ni neno lilitokana na neno la kihispania toka Marekani ya kusini na kati, "Uongozi binafsi." Ina maanisha jamii kujitawala yenyewe.  Angali Binafsi. . Angalia Utawala binafsi. Inamaanisha kuwa jamii imechukua hatamu kwenye utawala na katika kufanya maamuzi yatakayoleta maendeleo .
.
 (Deutsch: selbstverwaltung, English: auto management, Español: autogestión, Français: auto gestion, Português: auto gestão).
...
Uwezeshaji wa jamii:
...
Kuongeza uwezo wa jamii kuongeza uwezo wake wa kufanya jambo.
.
Ni zaidi ya kuongeza kazi ya kijamii, au huduma ya kijamii kama barabara, maji, elimu na huduma za afya.
.
kuongez auwezo na nguvu.inamaana stadi na maarifa zaidi na kuw amakini zaidi. haiwezi kuja kwa bahati au michango y amali ila kwa kuwezeshwa kupitia miradi ya kijamii, ila tu endapo wanajamii watahusishwa tokea mwanzo. ... Kuongeza demokrasia kutaisaidia serikali katika utawala na kuachia sehemu ya kutunga sheria kwenda kwenye jamii, mfano kufanya maamuzi juu ya maendeleo yake binafsi,- nguvu, uwezo nia. uwezeshwaji¨
.
 (Deutsch: gemeindestärkung, English: community empowerment, Español: potenciación comunitaria, Français: Renforcement communautaire, fortifier de la communauté, Português: fortalecendo da comunidade).
.
Uwezo:
.....
Exertion is needed to get stronger
Uwezo:
.....
Nia, nguvu au ushupavu wa jamii au ushirika.
..
(Deutsch:Macht, empowerment, die stärkung, leistungsfähigkeit, English: capacity, power, strength, Español: capacidad, potenciación,  Filipino/Tagalog: kakayahan, pagpapalakas, Français: capacité, empowerment, Italiano: empowerment, Kiswahili: uwezo, Português: capacidade, fortalecendo, Romãnã: capacitate, Pyccкий: paзвития, Somali: awooda).
.. 
Mwandishi Phil Bartle
Mtafsiri (translated by)
Alpha Mukama

––»«––
..
Maneno muhimu